R.KELLY ANAANDALIWA KESI NYINGINE KUBWA ZAIDI YA ALIZONAZO SASA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 9, 2019

R.KELLY ANAANDALIWA KESI NYINGINE KUBWA ZAIDI YA ALIZONAZO SASA


R. Kelly jana aliripoti mahakamani kwa ajili ya kutolea ushahidi video za ngono ambazo ziliwasilishwa na wanasheria kutoka kwenye mikono ya wasamaria wema.

Sasa wakati akiendelea kupambana na mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono taarifa mpya zinaeleza kuwa huwenda Kellz akafunguliwa mashtaka mengine makubwa zaidi hivi karibuni.

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Waendesha mashtaka wa mji wa Illinois watakaa kuanzia mwezi ujao kuzungumza na mashahidi wanaodai nguli huyo wa muziki aliwahi kufanya kosa la kuwasafirisha wasichana wadogo na kuwatumia kingono (Sex Trafficking), hivyo watazipitia tiketi za ndege pamoja na vyumba vya hoteli alizokuwa akiwafikisha.

Pia watazikusanya emails pamoja na meseji za kawaida ambazo zinaonesha namna alivyokuwa akiweka mitego ya kuwanasa ili kuwasafirisha. Ushahidi wa 'Physical' pia utatumika ikiwemo kuzifanyia uchunguzi nguo kama zina sampuli yoyote ya Uume wa staa huyo. 

Loading...

No comments: