SUDAN: OMAR AL-BASHIR KUHOJIWA KWA UTAKATISHAJI FEDHA NA KUFADHILI UGAIDI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 3, 2019

SUDAN: OMAR AL-BASHIR KUHOJIWA KWA UTAKATISHAJI FEDHA NA KUFADHILI UGAIDI


Habari kutoka nchini Sudan zinaeleza kuwa mwendesha Mashtaka mkuu ameamuru aliyekuwa Rais wa Taifa hilo ahojiwe kwa tuhuma za utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi. 

Uchunguzi wa tuhuma za utakatishaji wa fedha ulianza mara baada ya mamilioni ya dola za kimarekani kukutwa nyumbani kwa Al-Bashir

Inaelezwa kuwa vyanzo halisi vya fedha hizo havijulikani na ndio sababu ya Omar al-Bashir kuhojiwa

Aidha, Bashir pia anatuhumiwa kwa kutoa ufadhili wa fedha na silaha kwa makundi ya kigaidi ambayo bado hayajatajwa. 

Loading...

No comments: