TAASISI ZA KIDINI NA JUMUIYA ZA KIJAMII KUHAKIKIWA KUANZIA MEI 20

Taasisi za kidini


Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa taasisi zote za kidini pamoja na jumuiya za kijamii zinatakiwa kuhakikiwa upya. 

Awamu ya kwanza ya uhakiki itafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuanzia Mei 20 mpaka Mei 30. 

Nyaraka zinazohitajika katika uhakiki ni Cheti halisi cha usajili pamoja na kivuli chake, stakabadhi ya malipo ya mwisho ya ada, Katiba ya jumuiya/taasisi iliyopitishwa na msajili pamoja na barua ya uthibitisho kutoka kwa Afisa mtendaji wa kata/mtaa. 

Hii ndio barua rasmi yenye hii taarifa:


Post a Comment

0 Comments