NAJUTA KUJICHORA TATTOO-MONALISA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 2, 2019

NAJUTA KUJICHORA TATTOO-MONALISA

STAA wa filamu za Kibongo, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ , amesema anajutia maisha ya ujana aliyopitia yaliyomsababishia kujichora tattoo ambayo mpaka leo imekuwa ikimkera moyoni.

Yvonne Cherry ‘Monalisa’


Monalisa alisema tattoo aliyojichora enzi akiwa msichana imemuacha kwenye majuto, kwani sasa ndo ameanza kuona athari ya kujichora baada ya kuwa mtu mzima.

Alisema alama ya kopa na mkuki aliyojichora haifutiki na imekuwa ikimkera ambapo amejaribu kuchora ili kufunika mchoro huo, lakini bado imeshindikana, kitu ambacho kinamuumiza nafasi yake.

“Kila nikiitazama tottoo hii najutia kujichora, kweli ujana ni maji ya moto, sasa hivi najuta baada ya kuwa mtu mzima, nawashauri vijana waache kabisa mambo ya kujichora mwilini, watakuja kujutia kama nilivyo sasa,” alisema.


Yvonne Cherry ‘Monalisa’

Loading...

No comments: