TETEMEKO LA ARDHI LAIKUMBA PAPUA NEW GUINEA. HOFU YA TSUNAMI YAZUKA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 15, 2019

TETEMEKO LA ARDHI LAIKUMBA PAPUA NEW GUINEA. HOFU YA TSUNAMI YAZUKA

New Guinea Earthquake

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.7 kipimo cha richa, limetokea leo katika pwani ya kisiwa cha New Britain nchini Papua New Guinea na kuibua hofu ya kutokea tsunami katika pwani zilizopo Kilometa 1,000 kutoka kiini cha tetemeko hilo

Tetemeko hilo limetokea Kilometa 45 Kaskazini mwa mji mkuu wa New Britain, Kokopo na likiwa na kina cha Kilometa 10 na tahadhari ya kuwepo kwa tsunami imetolewa na Kituo cha Majanga ya Tsunami katika bahari ya Pacific

Hili ni tetemeko la ardhi la pili kuikumba Papua New Guinea ndani ya wiki moja ikiwa mnamo Mei 06, mwak huu tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.2 kipimo cha richa lilitokea na kusikila Kilometa 250 kutoka kwenye kiini

Aidha, katika mwezi Februari nchi hiyo ilikubwa na tetemeko la ardhi la ukubwa wa 6.4 na mwezi Machi tena lilitokea tetemeko lingine ka kubwa wa 6.1 kipimo cha richa.

Loading...

No comments: