TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMA: HAZARD, MATA, SESSEGNON, WAN-BISSAKA, DANILO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 3, 2019

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMA: HAZARD, MATA, SESSEGNON, WAN-BISSAKA, DANILO

Manchester United imemuongezea kiungo wa kati wa Uhispania Juan Mata, kandarasi ya mwaka mmoja huku ikiahidi kumuongezea tena mwaka mmoja wa ziada na inatumai kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 atasalia katika klabu hiyo. (Manchester Evening News)


Mchezaji wa Fulham Ryan Sessegnon, 18, anatarajia kujiunga na Tottenham mwisho wa msimu huu . (Mail)


Beki wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21, anasisitiza kuwa atasalia katika klabu hyo msimu ujao licha ya kuivutia klabu ya Manchester United. (London Evening Standard)
Beki wa Manchester City na Brazil Danilo, 27, amekubali kuandikisha mkataba wa kati ya miaka minne na mitano katika klabu ya Inter Milan ulio na thamani ya Yuro 3.5m kwa mwaka. (Gazetta dello Sport, via Manchester Evening News)


Beki wa Ajax na Uholanzi Matthijs de Ligt, 19, ana hamu ya kujiunga na klabu neyngine licha ya mazungumzo ya kuhamia Barcelona. (Mirror)

Atletico Madrid wamewasiliana na mchezaji wa Manchester City Nicolas Otamendi kuhusu uhamisho wa beki huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 31. (AS)
Manchester United inashindana na Juventus kumsaini beki wa Benfica na Ureno Ruben Dias, 21. (Record, via Manchester Evening News)


Arsenal imemuongeza beki wa Getafe Djene katika orodha yao ya wachezaji inayowamezea mate mwisho wa msimu huu . (Marca, via Mirror)
Qatar inafikiria kuhusu ushirikino wao na klabu ya Ufaransa Paris St-Germain baada ya klabu hiyo kufeli kupiga hatua zozote katika kombe la vilabu bingwa pamoja na matokeo mabaya katika fainali ya kombe la Ufaransa. (Le Parisien, via AS)

Crystal Palace na Burnley itamsaini winga wa Cardiff na Uingereza Josh Murphy, 24, iwapo klabu hiyo itashushwa daraja la ligi kuu ya Uingereza . (Football Insider, via Wales Online)
Mkufunzi wa Everton Marco Silva amepongeza tabia ya kiungo wa kati wa Senegal Idrisa Gueye, 29, ambaye alinyimwa uhamisho wa kuelekea Paris St-Germain mwezi Januari. (Liverpool Echo)


Winga wa Liverpool Ryan Kent, 22, aliyepo katika mkopo katika klabu ya Rangers, amethibitisha hamu yake kuondoka katika klabu ya Anfield , huku klabu hiyo ya Uskochi ikiwa na hamu ya kumsaini kwa kandarasi ya kudumu. (Express)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich hana hamu ya kuiuza klabu hiyo licha ya uvumi unaomuhusisha Muingereza tajiri Sir Jim Ratcliffe. (ESPN)


Mchezaji wa Chile Guillermo Maripan, 24, ambaye analengwa na West Ham, hatauzwa na Alavez mwisho wa msimu huu . (AS, via Inside Futbol)


Mkufunziwa zamani wa Everton, Manchester United na West Ham David Moyes angepenedelea kuifunza klabu badala ya timu ya taifa huku kukiwa na uvumi wa meneja huyo kuifunza timu ya taifa la Uskochi ama klabu ya Celtic. (Talksport)

Loading...

No comments: