Tigo na TECNO wazindua smart phone mpya aina ya Spark 3 na Spark Pro

Afisa mauzo kutoka kampuni ya tecno Mobile Tanzania Neema Khamis (kushoto) akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) simu mpya aina ya Tecno Spark Pro iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo Myonga (kushoto) na Meneja Uhusiano kwa umma wa kampuni ya Tecno Mobile Tanzania Eric Mkomoya.
 


 Mwandishi wa Habari kutoka Radio Times FM ya jijini Dar es Salaam Abdala Ally, akiwa katika picha ya pamoja na Meneja bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo Myonga (kushoto) na Meneja Uhusiano kwa umma wa kampuni ya Tecno Mobile Tanzania Eric Mkomoya (kulia) muda mfupi baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa kwa waandishi wa habari ambapo alifanikiwa kujishindia simu mpya ya kisasa ya Tecno Spark Pro iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
Meneja Bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo Myonga (kushoto) na Meneja Uhusino wa Kampuni ya kutengeneza simu ya Tecno Eric Mkomoya, wakionyesha simu janja za kisasa na za gharama nafuu aina ya Tecno Spark 3 na Tecno Spark 3 Pro zilizozindliwa jana jijini Dar es Salaam.

Meneja Bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo Myonga (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zimu janja mpya za kisasa na za gharama nafuu aina ya Tecno Spark 3 na Tecno Spark Pro jijini Dar es Salaam jan. Kulia ni Meneja Uhusiano kwa umma wa kampuni ya Tecno Mobile Tanzania Eric Mkomoya.
Nne.Afisa mauzo kutoka kampuni ya tecno Mobile Tanzania Neema Khamis 


Wateja kupata GB 96 ya intanet bure kwa mwaka 
Na MWANDISHI WETU 
Kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na TECNO leo wamezindua simu janja mpya aina ya TECNO Spark 3 na TECNO Spark 3 Pro zenye ubora wa hali ya juu na ukubwa wa inchi 6.2 itakayomwezesha wateja kuweza kufanya matumizi bora ya simu janja kwa bei nafuu kabisa.  
Wateja watakaonunua simu hizi pia wataweza kufurahia huduma ya mtandao wenye kasi kutoka Tigo pamoja na kifurushi cha GB 96 bure watakachoweza kutumia kwa mwaka mzima. 
Akizungumza wakati uzinduzi wa simu hizo, Meneja Bidhaa za Simu kutoka Tigo, Mkumbo Myonga, alisema Tigo inashirikiana na TECNO Mobile kuleta aina mbili za simu janja za TECNO Spark 3 katika soko la Tanzania ili kuwafanya wateja wake wafurahie maisha ya kidijitali. 
“Moja kati ya simu tunazozindua leo hii ina mfumo wa intanet wa 3G ambayo ni TECNO Spark 3. Simu hii inapatikana kwa bei ya Shilingi 280,000 tu na ya pili yenye mfumo wa intanet ya 4G inaitwa Spark 3 Pro, ikiwa inapatikana kwa Shilingi 333,000 tu. Simu zote hizi zinapatikana katika maduka yetu yote ya Tigo nchi nzima,” alisema Myonga.
Lengo la Tigo ni kuhamasisha maisha ya kidijitali katika jamii ya Kitanzania. Hii ndio sababu iliyowafanya kushirikiana na TECNO Mobile ili kuweza kuongeza idadi ya watumiaji wa simu janja na wa intanet katika soko la hapa nchini. Kampuni hii ya mawasiliano inaamini kuwa kushirikiana na watengenezaji wa simu ni mkakati unaoakisi lengo la kuwapatia Watanzania simu bora na za bei nafuu. 
Wakati huo huo, Meneja Mahusiano wa TECNO Mobile, Eric Mkomoya, alisema, “Ushirikiano wetu na Tigo umeleta mageuzi makubwa katika sekta ya mawasiliano ya kidijitali nchini Tanzania. Pamoja, tumeweza kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini kwa kuwapatia simu janja za kisasa na kwa bei nafuu. Kwahiyo, tunaamini ya kwamba simu hizi za TECNO Spark 3 ambazo tunazizindua hii leo zitaweza kutoa kiwango bora cha utumiaji kwa wateja wetu.”
Kwa maelezo ya Mkomoya, simu janja hizi pia zinakuja na kamera ya kiwango cha juu kabisa ambayo itawezesha wateja wanaopenda picha kuweza kupiga picha na video zenye mvuto na ubora wa juu. 
Simu ya TECNO Spark 3 inafanya kazi katika kiwango cha 3G intanet, ina kamera ya kisasa ya Mega Pixel 13, uwezo wa GB 16 ya RAM, na skrini ya nchini 6.2. Kifaa hiki pia kinaendeshwa kwa mfumo wa Android 9.0.
Kwa upande mwingine, simu ya TECNO Spark 3 Pro inafanya kazi katika kiwango cha 4G LTE ya intanet, ina kamera ya kisasa ya Mega Pixel 13, uwezo wa GB 32 ya Rom na GB 2 ya RAM, pamoja na na skrini ya nchini 6.2. 
Simu hizi zinakuja na waranti ya miezi 13.

Post a Comment

0 Comments