Ugonjwa wa Dengue wageuka tishio Tanzania, Fahamu dalili zake, jinsi ya kujikinga na maeneo yalioathirika zaidi DarUgonjwa wa Dengue umeendelea kuenea kwa kasi nchini Tanzania, ambapo kwa mujibu wa Wizara ya Afya mpaka sasa watu 12,000 wamegundulika kuugua ugonjwa tangu Januari mpaka mwezi Mei mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa wiki hii na Serikali kupitia wizara ya Afya inaeleza kuwa jumla ya wagonjwa 1,237 wamegundulika na ugonjwa huo katika kipindi tajwa huku jiji la Dar es Salaam likiongoza kwa kuwa na wagonjwa 1,150, Tanga wagonjwa 86 na Singida mgonjwa mmoja.
Je, Dalili zake ni zipi? kuna dalili nyingi ila hizi hapa chini ni miongoni mwa dalili hizo ambazo ndio za kwanza kujionesha kwa mtu mwenye homa ya Dengue.
  •           -Homa ya ghafla.
  •           -Kuumwa kichwa.
  •           -Uchovu.
  •           -Maumivu ya maungo na misuli.
  •           -Kichefu chefu na kutapika.
  •           -Maumivu ya macho.
  •           -Muwasho na vipele vidogo vidogo
Je, unaweza kujikinga na ugonjwa huu? Jibu ndio na hizi ndio njia za kujikinga na ugonjwa huo.
-Kuangamiza mazalia ya mbu.
-Kulala kwenye chandarua chenye dawa.
-Kuvaa nguo ndefu.
Kwa mkoa wa Dar Es Salaam ambao ndio umeathirika zaidi Tanzania, Haya ndio maeneo ambayo yameathirika zaidi.
Ilala, Kariakoo, Upanga, kisutu, Buguruni, Tabata, Mbezi, Ubungo, Kinondoni, Msasani na Masaki.
Homa ya dengue inaambukizwa na virusi vya mbu aina ya Aedes ambao ni weusi wenye madoadoa meupe yenye kung’aa. Dalili za ugonjwa huo huanza kujitokeza siku tatu mpaka 14 toka mtu alipoambukizwa.
ANGALIZO: Ukiona dalili zilizotajwa hapo juu au hata moja ya dalili zilizotajwa usimeze dawa yoyote nenda hospitali kamuona daktari.

Post a Comment

0 Comments