UINGEREZA: MAWAZIRI WAKUBALIANA KUHUSU SHERIA YA BREXIT - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 16, 2019

UINGEREZA: MAWAZIRI WAKUBALIANA KUHUSU SHERIA YA BREXIT


Mawaziri wa Uingereza wamekubaliana hii leo kuendeleza mazungumzo na chama cha upinzani cha Labour lakini wakiisisitiza serikali kuhakikisha sheria kuhusu nchi hiyo kujiondoa Umoja wa Ulaya ama Brexit inapitishwa kabla wabunge hawajekwenda kwenye mapumziko ya majira ya joto. 

Msemaji wa waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema baada ya kikao kirefu cha mawaziri wa May kwenye baraza hilo kwamba wamekubaliana hatua inayofuata lakini walielezea haja ya uharaka wa kupatikana kwa makubaliano ya kujiondoa yatakayopitishwa na bunge na kusainiwa kuwa sheria haraka iwezekanavyo. 

Amesema baraza hilo limekubali kuendelea na majadiliano na Labour kuangalia kinachowezekana. 

Loading...

No comments: