Ukosefu wa maamuzi ya kwenda kliniki chanzo cha vifo vya akina mama wajawazito - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, May 3, 2019

Ukosefu wa maamuzi ya kwenda kliniki chanzo cha vifo vya akina mama wajawazito

Dinah Atinda Mratibu wa Rmnch-UNFPA na huduma za uuguzi na ukunga- Tamisemi (Kushoto) Akiwa na Katibu tawala wa Mkoa SIMIYU - Jumanne Sagini

Washiriki waliohudhuria Uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze - Simiyu

Wawakilishi kutoka wizara ya afya wakiwa sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze - Simiyu 
Baadhi ya akina  mama katika halmashauri ya mji Bariadi hawana maamuzi ya kwenda hospitali kupata huduma za afya, wakisubiri ruhusa kutoka Kwa waume wao au wakwe zao.

Ukosefu Wa maamuzi pia unapelekea baadhi ya akina mama hao  kushindwa kupanga uzazi wa mpango mpaka wawaulize waume zao.

Akizungumza katika uzinduzi Wa kampeni ya ' Jiongeze Tuwavushe Salama katika mkoa wa Simiyu, Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto katika halmashauri ya Mji wa Bariadi, Frida Buyoga amesema ukosefu huo wa kutoa maamuzi umepelekea wengi wao kupoteza Maisha Kwa sababu ya kuchelewa kufika vituo vya Afya.

 Buyoga,  amesema hali hii imepelekea vifo vya vya akina mama 14 , kati ya 120 waliochelewa kufika vituo vya afya kwa sababu mbalimbali mwaka jana.

Licha ya akina mama hao kufariki, watoto wao waliokuwa bado hawajazaliwa (tumboni)  walikutwa hawachezi (wamefariki) baada ya kuchelewa kufika vituo vya Afya.

Amesema miongoni mwa sababu nyingine zinazopelekea baadhi ya akina mama  kuchelewa kufika vituo vya Afya ni pamoja na umbali Wa baadhi ya  vituo vya Afya, ambapo baadhi yao hulazimika kusafiri hadi kilometa 30 kwenda katika vituo vya Afya.

" Jitihada Kubwa zimefanyika kusaidia wajifungue Salama, ikiwemo ujenzi Wa zahanati na vituo vya Afya unaofanywa na serikali na wadau wa maendeleo.

Amesema katika halmashauri ya mji wa Bariadi, akina mama wastani 15-22 wanajifungua kila wiki , ikiwa ni ongezeko Kwa wanaokwenda kujifungua katika vituo vya Afya.

" Baadhi ya akina mama wamekuwa wakijifungua Nyumbani, lakini baada ya kuwapa elimu, wengi wao sasa hivi wanakwenda vituo vya Afya kujifungua na kupata huduma Kwa ajili yao na watoto wao, anasema Buyoga.

Amesema uzinduzi Wa kampeni ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' utasaidia sana kuelimisha akina mama kwenda katika vituo vya Afya, kujua Afya zao na kufuatilia chanjo zote muhimu, ili kujilinda wao na watoto wao.

Kampeni hii ipo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kitengo cha Elimu ya Afya Kwa Umma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo UNICEF

Loading...

No comments: