VIPODOZI VYENYE KEMIKALI YA KUJICHUBUA KUPIGWA MARUFUKU AFRIKA MASHARIKI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 15, 2019

VIPODOZI VYENYE KEMIKALI YA KUJICHUBUA KUPIGWA MARUFUKU AFRIKA MASHARIKI

Hydroquinone


Bunge la Afrika Mashariki (EALA) limepitisha azimio linalotoa wito wa kuwekwa kwa marufuku dhidi ya watengenezaji na waagizaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone.

Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni, mafuta na urembo wenye kemikali ya hydroquinone inayobadilisha ngozi kuwa nyeupe.

Hydroquinone ni kemikali inayopatikana katika aina mbali mbali za bidhaa mbali mbali za mwili ambayo kwa kawaida imetengenezwa kwa ajili ya kuifanya ngozi kuwa nyeupe.

"Athari za vipodozi vyenye hydroquinone zinaonekanana zimesambaa katika jumuiya nzima ya Afrika mashariki ," alisema Gideon Gatpan, mwanasheria kutoka Sudan Kusini.

Chini ya kipengele 81(2) cha mkataba ulioanzishwa na Jumuiya ya Afrika Mashrariki ,unaotambua umuhimu wa nchi wanachama katika kuweka viwango, na vipimo, wabunge wamependekeza Baraza la Mawaziri liundwe kwa ajili ya kuchunguza aina za kemikali zilizopo ndani yabidhaa za urembo kama moja ya viwango vya lazima katika kanda ya Afrika Mashariki.

"Baadhi ya bidhaa hizi huwa zina hadi 6% ya kemikali ya hydroquinone,"alisema mbunge kutoka Uganda Suzan Nakawuki.

Kenya na Rwanda, sawa na Afrika Kusini , Ghana na Ivory Coast , zimekwishaweka hatua za sheria za udhibiti au marufuku ya uagizwaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone.

Wataalamu wa masuala ya ngozi wanasema Kemikali ya hydroquinone inaweza kusababisha muwasho wa ngozi, mzio wa ngozi, kuchubuka kwa ngozi na kusababisha mabaka meusi na meupe na hata saratani ya ngozi.


NAMNA HYDROQUINONE INAVYOBADILI NGOZI:
Katika ngozi ya mwanadamu kuna chembechembe ambazo huitwa melanin. Kemikali ya Hydroquinone inakwenda kuzuia utengenezaji wa melanin kwenye mwili wako hivyo ngozi kupoteza rangi yake ya asili na ulinzi kutokana na miale ya jua yenye madhara Kazi ya chembe chembe hizi ni kuipa Rangi ngozi yako na kuilinda kutokana ni miale ya jua yenye madhara.

Loading...

No comments: