WANASIASA WAPIGWA MARUFUKU KUINGILIA WAUGUZI NA MADAKTARI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, May 9, 2019

WANASIASA WAPIGWA MARUFUKU KUINGILIA WAUGUZI NA MADAKTARI


Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepiga marufuku wanasiasa kuingilia fani za taaluma za madaktari, wakunga na wauguzi nchini.

Ummy ameyasema hayo bungeni juzi, Mei 7 wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya wizara yake, ambapo amesema kama daktari, muuguzi au mkunga amekosea wapelekwe kwenye mabaraza yao ambayo ndiyo yanashughulikia suala la nidhamu kwa kada hiyo ya wstumishi.

“Kutokana na hali halisi ilivyo, muuguzi mmoja anafanya kazi ambayo ingefanywa na wauguzi watano na madaktari wanafanya kazi hivyo si vema kuwakatisha tamaa.

“Sisi kwa kutambua umuhimu wao tutaendelea kuwatetea wauguzi na madaktari wetu, tusiwakatishe tamaa na isitoshe hao wenye fedha hawaendi kutibiwa kwenye hizo hospitali za Serikali, matokeo yake wanaoumia ni watanzania,” amesema Waziri Ummy. 

Loading...

No comments: