WAPIGANAJI 5 WA AL-SHABAAB WAJISALIMISHA KWA JESHI LA SOMALIA


Wizara ya habari ya Somalia imetangaza kuwa, wapiganaji watano wa kundi la al-Shabab akiwemo mtaalam mwandamizi wa mabomu wamejisalimisha kwa serikali ya Somalia wiki hii.

Wizara hiyo imesema Bw. Yusuf Ahmed Adow ambaye ni mtaalam wa mabomu wa kundi la al-Shabab amejisalimisha kwa Jeshi la taifa la Somalia SNA kwenye eneo la Gedo, kusini mwa nchi hiyo, na kufanya idadi ya watu waliosaliti kundi hilo kuongezeka hadi watano.

Maofisa wa mikoa ya nchi hiyo wamesema watu hao watakabidhiwa kwenye mamlaka ya Mogadishu.

Tukio hilo limetokea wakati wa operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi la al-Shabab linalojaribu kupinga serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa. 

Post a Comment

0 Comments