WEMA ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, May 14, 2019

WEMA ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI

Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu, leo jumanne tarehe 14, ameshindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kuhudhuria kesi inayomkabili ya kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo wakili wake Ruben Semwanza  ameeleza kuwa mshtakiwa huyo ni mgonjwa.


"taarifa nimepewa asubuhi hii nikiwa hapa mahakamani na mdhamini wake hayupo amenieleza yupo kikazi mkoani Arusha, hivyo naiomba Mahakama hii ipange tarehe nyingine," amedai wakili Semwanza.

Kwa upande wake Wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai kuwa shauri hilo lipo kwa ajili ya kusikilizwa pia shahidi aliyetakiwa awepo kutoa ushahidi.

Kesi hiyo imeahirisha kesi hiyo hadi Juni 11, 2019.
Loading...

No comments: