Wolper Afungukia Ishu ya Kukwea Pipa Mara Kwa Mara - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, May 8, 2019

Wolper Afungukia Ishu ya Kukwea Pipa Mara Kwa Mara

STAA wa Bongomovie, Jackline Wolper, amekata kiu ya mashabiki wengi wanaohoji safari zake za kila siku nje ya nchi kwa kusema anachofuata ni oda za bidhaa sambamba na kutangaza biashara zake.

Jackline Wolper,

Wolper alisema amekuwa akikutana na changamoto ya maswali kutoka kwa mashabiki wanaohoji kwanini anatumia pesa nyingi kustarehe nje ya nchi badala ya kufanya mambo ya msingi.

“Wengi wamekuwa wakinihukumu bila kujua ukweli wa ninachokwenda kufuata nje,ukiniona nasafiri ujue nipo kikazi zaidi, nimekuwa napata oda nyingi nchi mbalimbali na kunifanya kuonekana nipo bize sana, wakati mwingine nakwenda kwa ajili ya vipimo vya wateja wangu na kutangaza biashara, watu waelewe hivyo,î alisema Wolper.
Loading...

No comments: