Aslay Atoa Sababu za Kuvutiwa na Wema Sepetu Kwenye Filamu

Akiongea za gazeti la Mwananchi, mkali wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka amesema ikitokea akaingia kwenye ulingo wa uigizaji anatamani kufanya kazi na msanii wa filamu nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.

Akitaja sababu za kutamani kufanya kazi na staa huyo ni namna anavyomvutia jinsi anavyoigiza.
“Siku ikitokea nikajitosa kwenye filamu msanii wa kwanza kufanya naye kazi atakuwa Wema Sepetu na najua hiyo kazi itafanya vizuri sana sokoni, kwa sababu anajua na anauvaa uhusika haswa, ”anasema Aslya.
Aslay amefafanua kuwa anavutiwa na Wema akiwa anaigiza na si vinginevyo, hivyo kauli hiyo isitafsiriwe kwa mtazamo tofauti. Anasema ameliweka wazi hilo kwa sababu yeye ni msanii na ipo siku ataamua kufanya aina nyingine ya sanaa na msanii anayemkubali kwenye filamu ni huyo.

Post a Comment

0 Comments