BAJETI 2019/2020: KODI YA 'MAWIGI' KUPANDA, MUDA WA LESENI KUONGEZWA, KUFUTWA MSAMAHA WA KODI KWENYE TAULO ZA KIKE, NK


Hayo yamesemwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akiwa anatoa mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020

Amesema "Napendekeza kuongeza muda wa leseni za udereva kutoka miaka mitatu ya sasa hadi miaka mitano, napendekeza kuongeza tozo ya leseni ya udereva kutoka Tsh. 40,000 kwenda Tsh. 70,000."

Hata hivyo ameongeza kuwa Napendekeza kuongeza ada ya usajili wa magari 10,000 hadi 50000, bajaji kutoka 10,000 hadi 30,000 na pikipiki kutoka 10,000 hadi 20,000

Aidha katika hatua nyingine amesema kuwa "Napendekeza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nywele za bandia zinazotengenezwa nchini na asilimia 25 kwenye nywele bandia zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya Serikali."

Pia aliongelea Kufutwa kwa msamaha kodi ya ongezeko la thamani kwenye taulo za kike kwa kuwa haujawezesha kupatikana kwa bei nafuu kwa bidhaa hiyo muhimu kwa walengwa, badala yake ni kuwanufainisha wafanyabiashara. 

Hadi April 2019 Serikali imetoa Tril 5.4 kwa ajili ya miradi ya maendeleo Tril. 4.89 ni fedha za ndani na bilioni 500 ni fedha za nje, kiasi hiki hakijumuishi baadhi ya fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo

Katika bajeti ya mwaka 2018-2019 serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi Trilioni 32.48 kutoka katika vyanzo vyote vya ndani na nje, mchanganuo wa mapato yaliyopatikana hadi April, 2019 ni Trilioni 12.9 sawa na 87.4%

2018/19 maeneo yaliyopatiwa fedha ni mishahara kwa watumishi ni Tril. 6.3 zimelipwa , madeni ya Serikali Tril. 5.7, kuendeshaji wa ofisi tril. 4, mradi Umeme Rufiji Bil. 723.6 elimu bure na mikopo ya wanafunzi Bil 616, ununuzi wa ndege Bil. 200

Kati ya mwezi Julai 2018 na Aprili 2019, Serikali imegharamia miradi na matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Trilioni 6.3 ya mishahara, Trilioni 5.7 ya madeni ya nchi na Bilioni 616.9 ya Elimu bure na Mikopo ya Elimu ya Juu

Serikali itapunguza kiwango cha kodi kwa umeme unaouzwa kutoka Tanzania kwenda Zanzibar kutoka kwa asilimia 18, hadi 0 ili kuwapunguzia gharama za maisha kwa wananchi wa Zanzibar.

Kuna mafanikio katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, Ripoti ya Uwazi ya Kimataifa mwaka 2018 imeonesha Tanzania kuwa nafasi ya 16 kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara ikilinganishwa na nafasi ya 27 mwaka 2015

Shabaha za uchumi jumla katika kipindi hiki ni kukua kwa Pato la Taifa kwa 7.1% mwaka 2019 kutoka ukuaji halisi wa 7.0% mwaka 2018, Mfumuko wa bei kubaki kati ya 3.0% hadi 4.5% pamoja na mapato ya ndani kufikia 15.8%

"Napendekeza kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye makasha yenye majokofu yanayotumika kwenye kilimo cha kisasa cha mboga mboga kwa wakulima watakaoingiza makasha hayo kutoka nje ya nchi kwa matumizi ya kilimo"

"Napendekeza kutoza ushuru wa asilimia 35 badala ya 25 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za sausage na zinazofanana na hizo, pia kutoza kodi ya asilimia 35 badala ya 25 kwa nyanya zilizosindikwa (Tomato Sauce)"

Shabaha zingine za Serikali ni kuongeza mapato ya kodi hadi kufikia 13.1% ya Pato la Taifa kutoka 12.1%, matumizi ya Serikali kufikia 22.7% kutoka 21.6% na nakisi ya Bajeti inakadiriwa kufikia 2.3% ya Pato la Taifa kutoka 2.0% ya mwaka 2018/19

"Napendekeza kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa vilainishi vya ndege vinavyoingizwa nchini, tiketi za ndege, vipeperushi, kalenda, shajara, karatasi zenye nembo na sare za wafanyakazi zilizowekwa nembo ya Shirika"

"Napendekeza kufuta tozo ya asilimia 0.2 ya gharama ya mzigo na usafirishaji ya udhibiti wa vipodozi, vifaa tiba ikiwa ni pamoja na kondomu, mabomba ya sindano, gloves, pamba, na bendeji"

"Kufuatia mkutano wa Rais Magufuli na Wafanyabiashara uliofanyika Ikulu DSM, tumeazimia kufuta ada na tozo 54 zinazotozwa na Idara na Taasisi za fedha zinazojitegemea ili kuondoa kero kwa Wafanyabiashara"

Tozo zote zilizokuwa zinatozwa kwa Dola za Kimarekani zitatozwa kwa Shilingi ya Tanzania, isipokuwa kwa shehena za kemikali zinazokwenda nje ya nchi

"Napendekeza kufutwa kwa ada ya matumizi ya maji kwa watumiaji wenye visima nyumbani ambayo ilikuwa inatozwa kuanzia Shilingi 100,000 na kuendelea kulingana na matumizi ya maji"

"Napendekeza kuweka utaratibu mpya wa kuondoa mizigo bandarini ambapo wananchi wa kawaida wataruhusiwa kutoa mizigo yao bila ya kuwa na ulazima wa kutumia wakala wa forodha, utaratibu huu hautahusisha mizigo inayopitishwa hapa nchini kwenda nchi za nje"

"Serikali imeanzisha kitengo kipya cha kupokea malalamiko ya kodi na kitaratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, kitahusisha kupokea malalamiko kutoka kwa walipa kodi yakiwamo ya kuombwa rushwa na Watumishi wa Mamlaka ya Kodi TRA"

Kwa mwaka 2019/20 serikali inatarajia kukusanya na kutumia shilingi trilioni 33.11 Jumla ya mapato ya ndani (ikijumuisha mapato ya Halmashauri) yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 23.05/- sawa na asilimia 69.6 ya bajeti yote

Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya shilingi trilioni 19.10 sawa na asilimia 12.9 ya Pato la Taifa

Mapato yasiyo ya kodi kwa mwaka 2019/20 yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 3.18 na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni Shilingi bilioni 765.5

Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 4.96 kutoka soko la ndani. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 3.46 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva

Shilingi bilioni 1.50 sawa na 1.0% ya Pato la Taifa ni mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo

Kwa lengo la kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu, Serikali inatarajia kukopa trilioni 2.32 kutoka soko la nje kwa masharti ya kibiashara.

Tarehe 1 Julai, 2019 ndiyo siku ya kuanza kutekeleza hatua mpya za kodi zinazopendekezwa, Isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo. 

Post a Comment

0 Comments