Diamond Afungukia Sakata la Watoto, Amfagilia Hamisa Dhidi ya Zari

Akizungumza na wandishi wa habari leo, msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz anayetamba kwa sasa na kibao cha 'KANYAGA' amefungukia sakata juu ya malezi na mawasiliano na watoto wake na kusema amesema Hamisa Mobetto ni muelewa katika suala la mawasiliano ya mtoto wake kulinganisha Zari.


Diamond alisema Hamisa amekuwa muelewa ninapohitaji kuwa karibu na mtoto wake tofauti na Zari amekuwa mgumu tangu baada ya kuachana.

"Unajua mimi sio kwamba sipendi kuwasiliana na wanangu ila sema Zari ametumia fimbo ya kunichapa kupitia watoto, yaani hasira za kuachana mimi na yeye amezihamishia kwa watoto ndio maana amebiblock ili nisipate nawasiliano nao, lakini najua hii ni hasira na itaisha tu.

"Kwa sasa nimebaki na mawasiliano na mtoto wangu wa hapa Tanzania niliyezaa na Hamisa na nashukuru Hamisa kwenye hili amekuwa ni muelewa sana," alisema Diamond

Post a Comment

0 Comments