DRAKE AACHANA RASMI NA 'LEBO' ZA YOUNG MONEY & CASH MONEY

Msanii/Rapa Drake
Drake amemalizana na Young Money/ Cash Money Records baada ya kuitumikia kwa miaka 10? Majibu yamepatikana kupitia nyimbo hizi mpya mbili alizoziachia wikendi iliyopita. Drake ameziondoa Label hizo kwenye usimamizi wa Hatimiliki. 

Wataalamu wa mambo wanasema kwenye mitandao ya kusikiliza na kupakua nyimbo ya TIDAL, Spotify na Apple Music nyimbo hizo "Omerta na Money In The Grave" zilikuwa na alama ya hatimiliki (Copyright) ya Label hizo lakini jana Jumanne yalifanyika mabadiliko (Updates) na kuonekana zipo chini ya Frozen Moments. 

Frozen Moments ni kampuni ya Drake ambayo kwa miaka takribani 10 sasa amekuwa akiitumia kwenye kazi zake mbali mbali za Kibiashara. Japo haikuwa inasimamia masuala yake ya muziki isipokuwa wimbo wake na Summer Walker "Girls Need Love" wa mwaka 2018. 

Hii inaonesha kutimia kwa mistari yake kwenye wimbo wa "Is There More" uliopo kwenye album ya Scorpion ambapo alichana - Punde tu album hii ikidondoka nitakuwa nje ya mkataba "Soon as this album drop I'm out of the deal." ali-rap Drake ambaye alijiunga Young Money June 2009. 

Post a Comment

0 Comments