ED SHEERAN ATANGAZA UJIO WA ALBAMU MPYA MWEZI JULAI

No. 6 Collaborations Project
Ed Sheeran
Huyu ndio Ed Sheeran, baada ya albamu yake ya (÷), sasa anakuja na album mpya iitwayo (No. 6 Collaborations Project) ambayo ni album yake rasmi ya 4 na itajumuisha ushirikiano na wasanii mwanzo mwisho. 


Kwenye album hiyo yenye jumla ya ngoma 15, jana Ed Sheeran aliwataja wakali wa dunia kama Chance The Rapper, Camila Cabello, Cardi B, Travis Scott, Eminem, 50 Cent na wengine kibao. 


Ed Sheeran
Nyimbo za albamu hiyo mpya
No. 6 Collaborations Project ni muendelezo wa kuachia mradi huo ambao aliunzisha mwaka 2011 alipoachia No. 5 Collaborations Project ikiwa kama EP (Extended Play) japo haikubeba majina makubwa kwenye Collabo. 

Albamu hii mpya inatarajiwa kuachiwa Julai 12 mwaka huu. Mpo tayari kwa hii albamu? 

Post a Comment

0 Comments