Hakuna Mapenzi kwa Mastaa- Shilole

STAA wa filamu, mziki na mjasiriamali Zuwena Mohammed "Shilole" amefunguka kuwa, ukiwa na mahusiano na mtu star huwa hakuna mapenzi.

Akizungumza na EATV Shilole ambaye yupo katika ndoa na mume wake Uchebe, kwa mwaka wa pili sasa alifunguka; 

 "Inategemea mtu anataka mtu wa aina gani , kama mimi nilitaka mtu ambaye sio staa, ili niweze kuishi kwa raha, maana ukiwa na mahusiano na staa mtavimbiana , itakuwa sio sawa, hakuna mapenzi inakuwa mnaleteana maigizo". 

Kuhusu matumizi ya simu kati yake na mumewe, Shilole amesema huwa anashika sana simu ya mume wake, na kama siku akikuta meseji ya msanii yeyote wa kike katika DM ya Uchebe atamtaja live. 

Na Pia yeye na mume wake wanatumia simu moja kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram. 

Je wewe mpenzi msomaji unaweza kutumia simu moja na mwenzi wako?

Post a Comment

0 Comments