Hamisa Mobetto Afungukia Ishu ya Fobby - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, June 12, 2019

Hamisa Mobetto Afungukia Ishu ya Fobby

Mrembo mwenye vipaji vingi, Hamisa Mobetto amesema hakufurahishwa na lawama alizotupiwa na msanii Foby kuwa alikataa kufanya naye kolabo.Akizungumza na EATV, Hamisa amesema kuwa kutokuwepo kwake nchini wakati Foby anaomba kolabo ndiko kulisababisha mawasiliano kuwa magumu kati yako.

"Nilikuwa nje ya nchi wakati huo na alikuwa ananipigia simu akaniambia kuna nyimbo anataka tufanye nikamwambia nitumie nyimbo. Mimi nilishajiwekea kuwa kila anayeniandikia nyimbo kama ni msanii lazima nitafanya naye kolabo", amesema Hamisa.

"Sasa sielewi kitu gani kilimfanya afikirie kuwa nimekataa kufanya naye nyimbo. Sikuwahi kumpigia kumuuliza toka hapo kwa sababu nilikereka sana, ni bora angenipigia na kuniuliza kama nili'download' wimbo", ameongeza.

Msanii Foby ni moja kati ya watu waliomsaidia Hamisa kwenye kujifunza kuimba na kuingia kwenye Bongo Fleva, baada ya kuona kama anapotezewa na Hamisa aliamua kufunguka kuwa Hamisa amesahau fadhila baada ya kupokelewa vizuri kwenye muziki.
Loading...

No comments: