JAN OBLAK AOMBA KUONDOKA ATLETICO MADRID - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, June 11, 2019

JAN OBLAK AOMBA KUONDOKA ATLETICO MADRIDShirika la habari la ESPN limeripoti kuwa golikipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak ameomba kuondoka klabuni hapo baada ya kuvunjika kwa ahadi alizoahidiwa na klabu hiyo na anataka zaidi kuhamia Manchester United badala ya Paris Saint-Germain kama ilivyoripotiwa hapo awali. 

Wiki iliyopita Oblak alitoa maoni yake yaliyojaa wasiwasi kuhusu ushindani wa Atletico kwa msimu ujao ambapo wachezaji wa muhimu kama Griezmann anakaribia kuondoka pamoja na Luis Felipe, huku Lucas Hernandez, JuanFran na Diego Godin wakiwa tayari wameshaondoka klabuni hapo. 

Taarifa zinasema kwamba Oblak anataka kucheza kwenye Ligi kuu ya Uingereza licha ya kuwindwa sana na mabingwa wa ligi ya Ufaransa, PSG. 

Mustakabali wa De Gea bado upo gizani ndani ya United na yeye pia anahusishwa na kuhamia PSG, huku United wakiripotiwa kuwa tayari kutoa Euro Milioni 120 ambayo ni thamani ya Oblak kwenye mkataba wake kama De Gea ataondoka Old Trafford. 

Loading...

No comments: