MAN CITY HATARINI KUIKOSA CHAMPIONS LEAGUE MSIMU UJAO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 13, 2019

MAN CITY HATARINI KUIKOSA CHAMPIONS LEAGUE MSIMU UJAO


Hali si shwari kwa mabingwa wa Ligi kuu ya Uingereza, Manchester City ambao wako katika hatihati ya kukosa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (Champions League) kwa msimu unaofuata. 

City wanashutumiwa kuvunja sheria ya 'Financial Fair Play', kwa maana ya ulinganifu mapato na matumizi yao. 

Mabingwa hao wanashutumiwa kufanya udanganyifu kuhusu pesa wanazopata kutokana na mikataba ya wadhamini lakini kwa mujibu wa UEFA ni kuwa wahisani wa fedha hizo ndio hao hao wamiliki wa timu na wala sio wadhamini. 

Licha ya City kupeleka rufaa yao kwenye mahakama ya usuluhishi wa michezo (CAS) na wamekiri kupokea rufaa hiyo, bado UEFA wameshikilia msimamo na adhabu hiyo huenda ikatolewa hivi karibuni. 

Loading...

No comments: