Maneno ya AY na Mwana FA kwa Jaguar

Wasanii wa Bongo Fleva Ambwene Allen Yessayah ‘AY’  na Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ wamemshauri Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi 'Jaguar' kuwaomba msamaha kutokana na kauli za kibaguzi alizozitoa.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram, AY ambaye ameshawahi kufanya kazi za kisanii na  Jaguar ameandika;

“Jaguar mimi Nawajua Watanzania wenzangu kuliko wewe tumia maneno haya muhimu kuwaambia wananchi hii issue iishe tuendelee na mambo mengine..Sema hivi- SAMAHANI...NIMEKOSA...NIMEKOMA ... NA SITARUDIA TENA -Ni mimi mshkaji wako Ambwene Allen Yessayah (A.Y)".

Kwa upande wake Mwana FA ameandika “My brother Jaguar ipo hekima kwenye kugundua ulikosea na kuomba radhi,uliteleza tu..apologize and lets move on,kila mtu hukosea..hii ya kuzunguka zunguka na maneno haitasaidia,haitaondoa hii kitu.. How did we misinterpret “tutawapiga”?"

Jaguar alikamatwa jana na maafisa wa polisi katika viwanja vya Bunge kufuatia kauli yake ya kibaguzi juu ya raia wa kigeni wanaofanya kazi na biashara nchini humo.

Leo June 27, 2019 amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kutoa kauli za kichochezi dhidi ya Wafanyabiashara wa kigeni wakiwemo Watanzania.

Post a Comment

0 Comments