MGOGORO SUDAN: MAUAJI, UBAKAJI, NA WATU KUTOWEKA VYASHAMIRI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, June 13, 2019

MGOGORO SUDAN: MAUAJI, UBAKAJI, NA WATU KUTOWEKA VYASHAMIRI


Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa zaidi ya 129 wameuawa wakati jeshi likidhibiti maandamano dhidi ya Serikali, wakati huo huo taarifa zisizo rasmi zinadai watu 500 wameuawa

Watu zaidi ya 700 wamejeruhiwa katika ghasia zinazoendelea nchini humo huku waliobakwa ni takribani watu 70

Maelfu ya watu wanadaiwa kutoweka huku wengi wao wakidaiwa Kukamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama

Taifa hilo linaongozwa na jeshi baada ya aliyekuwa Rais Omar al Bashir kuondolewa kwa shinikizo la maandamano ya Wananchi

Kwa sasa wananchi wanalitaka jeshi kuitisha uchaguzi ili kurudisha madaraka kwa raia. 

Loading...

No comments: