Natasha wa Diamond Kuishangilia Taifa Stars Kesho Dhidi ya Kenya

STAA wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa mpenzi wake mama kijacho Tanasha Donna Oketch ambaye ni raia wa Kenya ataishabikia  timu ya Tanzania hapo kesho itakapocheza mechi ya Afcon dhidi ya Kenya. 

Diamond Platnumz na Tanasha

Diamond amesema hayo jana alipokuwa akitangaza kuzindua rasmi tamasha la Wasafi linalotarajia kuanza Julai 12, 2019.

Amesema wakati wa kuwania kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliifunga timu ya mashemeji zake Uganda, lakini safari hii kwa mara ya kwanza atambadili uraia mpenzi wake huyo kutoka Kenya kwa kumshawishi ashangilie timu ya Tanzania.

“Atavaa jezi ya Tanzania na ataishangilia Taifa Stars, nitamshawishi, msiwe na hofu wifi yenu atawaunga mkono,” alisema Diamond.

Alipoulizwa kuhusu lini atafunga ndoa na mwanadada huyo baada ya kuwa ameshapata watoto na wanawake wawili tofauti na tayari huyo pia ni mama ijacho alijibu.

Badala ya kujibu alisema: “Subirini. Nimewaambia Julai 7, 2019 kutakuwa na tukio kubwa maeneo ya Mwenge Mwenge hapo, meza zitakuwa 10 tu meza tano zitauzwa Sh 500,000 kila moja.”

Post a Comment

0 Comments