RAIS WA DRC KUFIKA NCHINI LEO KWA AJILI YA ZIARA


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi anatarajiwa kuwasili nchini leo Alhamisi, Juni 13 kwa ajili ya ziara ya siku mbili

Siku chache zilizopita Rais Tshisekedi aliandika barua kwenda kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika Mashariki akiwasilisha ombi la nchi yake kuwa mwananchama wa umoja huo. 

Tshisekedi alichaguliwa kuwa Rais wa DRC Januari mwaka huu akichukua nafasi ya Joseph Kabila. 

Post a Comment

0 Comments