Loading...

Tetesi za soka Ulaya Leo: Guardiola, Sarri, Pogba, Rakitic, Wan-Bissaka, Maguire, de Ligt, Lampard, Onana, Buffon

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anaangalia uwezekano wa kuchukua mapumziko ya muda katika soka mwishoni mwa msimu ujao ikiwa atashinda Championi Ligi . (Star)


Manchester United wamefanya mawasiliano na kiungo wa kati wa Barcelona Mcroatian Ivan Rakitic mwenye umri wa miaka 31. (Sport - in Spanish)

United watatakiwa kuvunja mikataba miwili ya rekodi ya uhamisho wa mchezaji wa safu ya ulinzi, ikiwa watahitaji kusaini mkataba na wachezaji wa safu hiyo kutoka England Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21, kutoka Crystal Palace na Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Leicester watakaolipwa pamoja pauni milioni 130. (Standard)

Hata hivyo , United wanataka sana kusaini mkataba na mchezaji wa timu ya England ya Norwich City anayecheza safu ya ulinzi Max Aarons,mwenye umri wa miaka 19, ikiwa azma yao ya kumchukua Wan-Bissaka itafanikiwa. (Sky Sports)

Mlinzi wa klabu ya Ajax ya Uholanzi Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19, anasema " hajui moyo wake unasema nini " lakini ataamua juu ya hali yake ya baadae atakapokuwa mbali likizoni . (Mundo Deportivo - in Spanish)

Washauri wa De Ligt wamemwambia aende katika timu kama Manchester United ambako anakuwa na hakikisho la kuanza , kabla ya kuhamia Barcelona baadae katika taaluma yake (Sport)

Chelsea wameanzisha mazungumzo na meneja wa Derby Frank Lampard juu ya kurejea katika Stamford Bridge kwa kiungo huyo wa zamani wa kati wa Blues.(Mail)

Chelsea wanataka Meneja atakayechukua nafasi ya Maurizio Sarri anayeongoza timu hiyo ambaye tayari anatarajia kuhamia katika klabu ya Italia ya Juventus baadae wiki hii. (Mirror)

Real Madrid watafanya kila wawezalo kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, mwenye umr wa miaka 26, kwani ndio chaguo la kwanza la Zinedine Zidane (Marca)

West Ham wanamlenga mchezaji wa safu ya kati ya timu ya Villarreal ya Uhispania Pablo Fornals, mwenye umri wa miaka 23, Baada ya kutuliza haja yao kwa kiungo wa kati wa Celta Vigo Mslovakia Stanislav Lobotka, mwenye umri wa miaka 24. (Guardian)

Mlindalango wa Utaliano Gianluigi Buffon, mwenye umri wa miaka 41, anaweza kujiunga na Porto baada ya kuondoka Paris St-Germain, kuchukua nafasi ya Spaniard Iker Casillas, mwenye umri wa miaka 38. (Tuttosport - in Italian)

Manchester United watamuangalia mlindalango wa Ajax Mcameroon Andre Onana, mwenye umri wa miaka 23,ikiwa Muhispania David de Gea, mwenye umri wa miaka 28, ataondoka kikosini msimu huu. (Independent)

Barcelona wanatumai kujiingizia takriban Euro milioni 60 kutokana na mauzo ya wachezaji kabla ya Juni 30 kwa lengo la kuweka uwiano wa mahesabu ya akunti kwa ajili ya msimu wa 2018-19. (ESPN)

Washindi hao wa Ligi ya Uhispania wanamtaka mshambuliaji Louie Barry wa West Brom mwenye umri wa miaka 15 aliyeko katika kikosi cha Timu ya England ya walio na umri wa chini ya miaka 16. (Birmingham Mail )

Kiungo wa kati wa England Alex Oxlade-Chamberlain, mwenye umri wa miaka 25, anapanga kurefusha mkataba wake wa sasa na Liverpool hadi 2023. (Mail)

Mshambuliaji wa timu ya Benfica ya Ureno Joao Felix, mwenye umri wa miaka 19, anataka kuhamia Atletico Madrid. (AS - in Spanish)

Manchester United wanafanya mazungumzo ya kumuuza mchezaji wa safu ya nyuma Mtaliano Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29, huku Valencia na klabu nyingine mbili za Italia ambazo hazikutajwa zikimtaka. (ESPN)

Mkurugenzi wa Boca Juniors Nicolas Burdisso ana matumaini ya kumleta iungo wa kati wa zamani wa Roma na Italia Daniele de Rossi, mwenye umri wa miaka 35, katika klabu ya Argentina, licha ya ripoti kuwa amepanga kujiunga na upande wa ligi ya MLS katika kikosi cha Los Angeles FC. (Closs Continental via Yahoo)

Mlindalango wa Costa Rica Keylor Navas, mwenye umri wa miaka 32, anataka Real Madrid imlipe miaka miwili aliyobakiza ya mkataba wake na imuache aende msimu huu wa miaka miwili, lakini klabu hiyo inataka ilipwe euro milioni 20 kwa yeyote atakatemtaka mchezaji huyo . (AS - in Spanish)

Kiungo wa kati wa West Ham' Muingereza Jack Wilshere, mwenye umri wa miaka 27, anaangalia uwezekano wa kustaafu huku akiendelea kupona jeraha alilopata wakati wa mechi na Arsenal, maana ugonjwa wa mtoto wake wa kiume umemfanya ''asahau soka'' . (Athletes Stance)

Post a Comment

0 Comments