TYGA AZUNGUMZIA UMUHIMU NA NAFASI YA LIL WAYNE KWENYE MUZIKI NA MAISHA YAKE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, June 11, 2019

TYGA AZUNGUMZIA UMUHIMU NA NAFASI YA LIL WAYNE KWENYE MUZIKI NA MAISHA YAKE


Tyga ni moja kati ya mazao ya Lil Wayne, alimsaini na kumtambulisha rasmi kwenye muziki kipindi ana umri wa miaka 17. Leo Tyga ameachia album yake ya 7 (Legendary) ndani amemshirikisha Wayne.

Kwenye mahojiano na Ebro Darden wa Beats 1 Radio, Tyga alizungumzia kulelewa na Lil Wayne kimuziki ikiwemo kupata ushawishi mkubwa wa kufanya anachokifanya sasa. 

"Alinisaidia kukua na kuwa hivi nilivyo, alinishawishi na kunifunza kwa miaka mingi. Alinisaini nikiwa na umri wa miaka 17. Nilikuwepo wakati anaitengeneza Carter III, nina mtu ambaye nina mtazama kwa kila kitu kuanzia kuingia studio, kufanya shows. Nimeamua kumuweka mwanzoni kabisa mwa album yangu." alisema Tyga.

Legendary ilitoka June 7 mwaka huu na tayari imethibitishwa kuuza kiwango cha Gold siku hiyo hiyo ilipoachiwa rasmi. Wayne amekula shavu kwenye wimbo uitwao "On Me" na pia kuna wimbo unaitwa "Lightskin Lil Wayne".

No comments: