ULEVI NA UZEMBE WACHANGIA ASILIMIA 76 YA AJALI ZA BARABARANI


Imeelezwa kuwa moja ya chanzo kikuu cha ajali za barabarani hususan kwa waendesha bodaboda ni makosa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na ulevi na uzembe ambao huchangia kwa asilimia 76%.

Hayo yamesemwa jana Juni 13,2019 na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Musoma Mjini, Vedastus Mathayo Manyinyi aliyehoji licha ya kazi nzuri ya waendesha bodaboda ya kurahisisha usafiri na kupunguza tatizo la ajira ,bado ziko changamoto mbalimbali wanazosababisha kama ajali za mara kwa mara pamoja na wizi ,nini mkakati wa serikali kupunguza tatizo hilo.

Katika majibu yake Mhandisi Masauni amesema vipo vyanzo vikuu vitatu vinavyosababisha ajali za barabarani hapa nchini ikiwa ni pamoja na makosa ya kibinadamu ambayo huchangia kwa asilimia 76%,ubovu wa Magari asilimia 16%, mazingira ya Barabara asilimia 8%.

Mhandisi Masauni ameyataja baadhi ya makosa ya kibinadamu ni pamoja na ulevi,uendeshaji wa kizembe,mwendokasi,uzembe wa waendesha pikipiki,uzembe wa waendesha baiskeli,uzembe wa watembea kwa miguu.

Aidha,Serikali kupitia jeshi la polisi hapa nchini imekuwa ikitoa elimu kwa waendesha bodaboda namna nzuri ya utumiaji wa pikipiki ikiwa ni pamoja na kuvaa kofia ngumu ,kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa leseni kwa waendesha bodaboda ili kupunguza waendeshashaji wasio na leseni na wanaoweza kusababisha ajali. 

Post a Comment

0 Comments