UWANJA WA NDEGE SAUDI ARABIA WASHAMBULIWA NA WAASI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, June 11, 2019

UWANJA WA NDEGE SAUDI ARABIA WASHAMBULIWA NA WAASIHarakati ya Ansarullah nchini Yemen imetangaza kuwa imeshambulia uwanja wa ndege wa Jazan huko kusini magharibi mwa Saudi Arabia kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Shambulizi hilo linatajwa kuwa la tano la aina yake la Ansarullah dhidi ya Saudi Arabia katika wiki za hivi karibuni.

Televisheni ya al Masiira imelinukuu Jeshi la anga la Yemen likisema kuwa, mashambulizi hayo yamelenga uwanja na maegesho ya ndege zisizo na rubani zinazotumiwa na Saudi Arabia dhidi ya taifa la Yemen.

Wapiganaji wa Ansarullah wamezidisha mashambulizi yao dhidi ya Saudia katika wiki za hivi karibuni na Jumatano iliyopita waliteka vituo 20 vya jeshi la nchi hiyo katika eneo la Najran huko kusini mwa Saudia.

Wiki tatu zilizopita ndege zisizo na rubani za Ansarullah zilifanya mashambulizi manne ya ndege zisizo na rubani ambayo yalilenga mfumo wa kujikinga na makombora wa Patriot na kambi ya kijeshi ya eneo la Najran.

Makamanda wa harakati ya Ansarulla nchini Yemen wanasema kuwa mashambulizi hayo ni jibu la jinai na mauaji yanayoendelea kufanywa na watawala wa Saudia na waitifaki wao dhidi ya raia wasio na hatia wa Yemen.

Mwezi uliopita harakati hiyo pia ilishambulizi mabomba makubwa zaidi ya kusafirisha mafuta ya Saudi Arabia na kusitisha usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu kwa utawala huo kwa masaa mengi.

Maelfu ya raia wa Yemen wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na hujuma na mashambulizi ya Saudi Arabia, Imarati na waitifaki wao dhidi ya taifa la Yemen.
Loading...

No comments: