CHUKUA HII: LEBRON ALIWAHI KUKATAA DILI LA $10M HUKU FAMILIA YAKE IKIWA HOI KIFEDHA
Akiwa na umri wa miaka 13 tu Lebron James akiwa High School alikutana na matajiri toka kampuni ya Reebok na walimuahidi kumpatia ($10 million) sawa na TZS Bilioni 20 kwa sasa ili asiingie makubaliano na kampuni yoyote ya viatu ikiwemo Nike na Adidas.

Lakini huwezi kuamini, Lebron aliipiga chini Ofa hiyo huku familia yake ikiwa na dhiki na kodi ya nyumba waliyokuwa wamepanga ilikuwa ni ($17) sawa TZS Elfu 40 kwa mwezi.

Aliwahi kuzungumza kuwa aliamini kama Reebok wamempatia ofa hiyo basi makampuni mengine hayatoshindwa kumpa zaidi. 

Na kweli bwana, miaka mitano baadaye alipofikisha umri wa miaka 18 alisaini dili lake la kwanza na kampuni ya NIKE lenye thamani ya ($90 million) sawa TZS Bilioni 200.

Mwaka 2015, Lebron James alisaini tena dili jipya na NIKE, hili lilikuwa la maisha ambapo thamani yake ni ($1 Billion) sawa na TZS 2 Trilioni. 

Post a Comment

0 Comments