JAY Z AGEUKIA BIASHARA YA BANGI SASA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, July 10, 2019

JAY Z AGEUKIA BIASHARA YA BANGI SASA


Mwezi mmoja baada ya kutangazwa kuwa ameufikia utajiri wa ($1 Billion) na Jarida la Forbes kutokana na uwekezaji wake kwenye biashara mbali mbali, Jay-Z ameonekana kuongeza biashara nyingine na sasa ni BANGI.Mtandao wa XXL umetanabaisha kuwa jana Jumanne Jay-Z alitangaza kuungana kibiashara na kampuni ya Caliva ya mjini California kama Mwana Mkakati/Mipango Mkuu wa Chapa hiyo (Chief Brand Strategist) kazi yake kubwa itakuwa kukuza na kuistawisha chapa ya kampuni na pia kusaidia kushawishi kiuhalali watu kwenye kukuza kiwanda cha Bangi.

Kwenye maelezo yake Jay-Z alisema; "Kila ninachokifanya nakifanya kwa usahihi na katika kiwango cha juu sana, kwa nguvu kubwa waliyonayo kwenye ulimwengu wa biashara ya Bangi, tunataka kutengeneza kitu bora sana kwa ajili ya watu."

Loading...

No comments: