Magufuli Atoa Maagizo kwa Dk Kigwangalla, Ampongeza Faru Rajabu - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, July 9, 2019

Magufuli Atoa Maagizo kwa Dk Kigwangalla, Ampongeza Faru Rajabu

Akiongea leo  Jumanne Julai 9, 2019 wakati wa uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato mkoani Geita,  Rais wa Tanzania, John Magufuli ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii inayoongozwa na Dk Hamisi Kigwangalla kutatua changamoto za gharama kubwa za utalii na usafi katika hoteli zinazowahudumia watalii.


Rais wa Tanzania, John Magufuli

Magufuli amesema wizara hiyo inayoongozwa na Dk Hamis Kigwangalla inapaswa kuwa na mkakati madhubuti wa kuongeza idadi ya watalii hapa nchini ambao kwa mwaka 2018 walifikia milioni 1.5.

"Miongoni mwa malalamiko ninayoyapata kupitia ripoti ya robo mwaka ya mabalozi ni gharama kubwa za utalii na usafi wa hoteli, hamna budi ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo fanyeni ziara za mara kwa mara," amesema Magufuli.

Ameitaka wizara hiyo kuhamasisha utalii wa ndani kwa kupunguza gharama za utalii huku akitolea mfano wa nchi ya Moroco na Misiri zinapokea watalii zaidi ya milioni 10 kwa mwaka lakini Tanzania ya pili kwa wingi wa vivutio duniani inapokea watalii milioni moja tu.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemwagia sifa faru Rajabu kwa kazi nzuri aliyoifanya.

''Hakuna budi kupongeza kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na faru rajabu, mtoto wa faru John naambiwa kwasasa amezalisha watoto 40, nadhani wajina wangu john alikuwa hajitumi vizuri''.

Rais Magufuli amemuagiza waziri wa Maliasili, kuhakikisha anawachukulia hatua stahiki viongozi wa Maliasili, ikiwemo kuwafukuza kazi, endapo itatokea upotevu wa wanyama katika hifadhi mbalimbali za wanyama.

Aidha wakati wa Uzinduzi huo, Rais Magufuli amekabidhiwa tuzo mbili, ikiwemo ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, pamoja na zawadi ya Taswira ya Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere, kama zawadi ya kumthamini na kuutambua mchango wake wa Uhifadhi wa Mazingira.
Loading...

No comments: