MAREKANI KUUNDA MUUNGANO WA MATAIFA DHIDI YA VITISHO VYA IRAN

Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Marekani amesema Washington itaendelea na mipango ya kuunda muungano wa mataifa ili kufutialia na kukabiliana na vitisho vya Iran dhidi ya shughuli za usafirishaji katika eneo la ghuba na mlango bahari muhimu wa Hormuz.Jenerali Joseph Dunford ambaye ni mwenyekiti wa wakuu wa vyombo vya usalama nchini Marekani, amesema kuwa tayari wameandaa mpango mahsusi na katika wiki chache zijazo itakuwa wazi ni mataifa yapi yatajiunga na juhudi hizo za Marekani.

Afisa huyo amearifu pia kuwa amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo na kaimu waziri wa Ulinzi Mark Esper kuhusiana na mipango hiyo.Juhudi hizo za Marekani zinafuatia wasiwasi wa utawala wa rais Donald Trump kwamba Iran ndiyo iliongoza mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya meli za mafuta katika eneo la ghuba.

Post a Comment

0 Comments