NICKI MINAJ AAMUA KUIFUTA SHOW YAKE YA SAUDI ARABIA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, July 10, 2019

NICKI MINAJ AAMUA KUIFUTA SHOW YAKE YA SAUDI ARABIA


Baada ya maneno mazito na mashambulizi ya mtandaoni hatimaye Nicki Minaj ameamua kuifuta show yake ya nchini Saudi Arabia.Hii imekuja baada ya msukumo toka kwenye taasisi isiyo ya Kiserikali ambayo inajihusisha na mambo ya Haki za Binadamu kumtaka Nicki Minaj kujitoa kwenye tamasha hilo liitwalo Jeddah World Fest.

Leo asubuhi Minaj amekubali hilo na kuandika ujumbe kwenye Ukurasa wake instagram kwamba amesikia sauti za watu wa Saudi Arabia na kwa upendo kabisa ameamua kuziitikia.

Hii imekuja baada ya wananchi wa taifa hilo kupinga vikali ujio wa msanii huyo kwani kwa muonekano wake na aina ya nyimbo zake ni kinyume na sharia zao na Utamaduni.
Loading...

No comments: