Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika kwa msimu wa 2019/20 yatoka, kazi kwa Simba na Yanga sasa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, July 22, 2019

Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika kwa msimu wa 2019/20 yatoka, kazi kwa Simba na Yanga sasa
Shirikisho la soka la Afrika (CAF) jana limetoa ratiba ya mechi za hatua ya awali katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa msimu mpya wa 2019/20.

Klabu ya Simba SC imepangwa kucheza na UD do Songo ya Msumbiji huku Klabu ya Yanga SC ikipangwa kucheza na Township Rollers ya Botswana.

Katika mechi hizo, Yanga wataanzia nyumbani na Simba wataanzia ugenini.

Mechi za kwanza za hatua hiyo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 9,10,na 11 na marudiano zitachezwa Agosti 23,24,na 25.

Endapo timu hizo za Tanzania zikipita hatua hiyo awali na kufuzu katika raundi ya kwanza ,Simba itakutana na mshindi kati ya Nyasa Big Bullets na FC Platnum, na Yanga atakutana na mshindi kati ya Green Mamba na Zesco United. 

Loading...

No comments: