Ray Kigosi: Jaden Amenipa Heshima - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, July 22, 2019

Ray Kigosi: Jaden Amenipa Heshima

STAA wa Bongo Movie, Vicent Kigosi ‘Ray’ amesema mwanaye wa kiume, Jaden amekuwa akimtoa machozi ya furaha kutokana na heshima ya kuitwa baba aliyonayo.
Vicent Kigosi ‘Ray’ na Jaden
Akizungumza na gazeti moja hivi karibuni, Ray alisema, mtoto wake huyo amempa alama isiyofutika katika maisha yake kwani kuitwa baba ni jambo zito ambalo mtu anapaswa kujivunia.

Ray alisema, amekuwa akitembea kifua mbele kutokana na uwepo wa Jaden kwani amempa chapa na heshima mbele ya jamiii.

“Hivi unajisikiaje mtoto wako umliyezaa anafanana na wewe kila kitu, kwangu hili limekuwa likinipa furaha inayonitoa machoni lakini kingine mwanangu amenipa heshima ambayo sijaipata miaka yote nadiriki kusema Jayden wangu amenipiga chapa ya ushujaa,” alisema Ray.
Loading...

No comments: