VAR KUANZA KUTUMIKA RASMI LEO KWENYE MECHI ZA AFCON 2019 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, July 10, 2019

VAR KUANZA KUTUMIKA RASMI LEO KWENYE MECHI ZA AFCON 2019


Teknolojia ya uamuzi kwa kuchambua video maarufu kama VAR itaanza kutumika leo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Mataifa Afrika 2019.Hii ni mara ya kwanza teknolojia hiyo kutumika katika michuano hii.

Awali ilipangwa kuanza kutumika kuanzia katika hatua ya nusu fainali lakini ikabadilishwa na sasa itaanza kutumika kuanzia robo fainali.

Mechi za robo fainali zikatazochezwa leo ni Senegal dhidi ya Benin saa moja kamili usiku na Nigeria dhidi ya Afrika Kusini kuanzia saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki. 

Loading...

No comments: