Vodacom yatoa mchango wa madawati 300 kwa wanafunzi 400 katika wilaya ya Bariad - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, July 12, 2019

Vodacom yatoa mchango wa madawati 300 kwa wanafunzi 400 katika wilaya ya Bariad


 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga (Kushoto) akipeana mkono na Meneja mauzo mwandamizi wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa, Ahmed Akberali (Kulia) katika hafla ya kukabidhi madawati 300 yenye thamani ya TZS millioni 61 yaliyotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya shule ya msingi ya Salunda na Somanda jana, Dutwa wilayani humo. Taasisi hiyo imetoa msaada wa madawati ikiwa  ni njia mojawapo ya kuisaidia serikali kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi nchini.


Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Salunda na Somanda wakiwa wamekalia madawati yaliyokabidhiwa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, jana wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Taasisi hiyo imetoa madawati 300 yenye thamani ya TZS milioni 61 kwa shule hizo ikiwa ni njia mojawapo ya kuisaidia serikali kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi nchini.


Loading...

No comments: