WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU WAMTAKA NICKI MINAJ KUTOFANYA SHOW SAUDI ARABIA
Kundi la Haki za Binadamu limemuandikia barua Nicki Minaj likimtaka kuahirisha kushiriki tamasha lililoandaliwa na Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman maarufu kama MBS.

The Human Rights Foundation limemtaka rapa huyo wa kike kutoka Marekani kutohudhuria tamasha hilo liitwalo Jedah World Fest litakalofanyika Julai 18, 2019 na badala yake aungane nao kwakuwa wanaichukulia Serikali ya nchi hiyo kama Serikali inayokiuka haki za binadamu kwa kiwango cha juu.

Kupitia barua hiyo, wamemuomba arudishe fedha walizompa na atoe tamko la kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na kuitaka Serikali kuwaachia huru wanawake wanaharakati wa Saudi Arabia wanaoshikiliwa gerezani.

Hadi sasa, bado Nicki hajatoa majibu yoyote kuhusu kushiriki au kutoshoriki tamasha hilo la Mwana wa Mfalme.

Post a Comment

0 Comments