ACACIA YARUHUSIWA KUENDELEA KUSAFIRISHA DHAHABU


Kampuni ya Acacia imeruhusiwa kuendelea na utaratibu wa kusafirisha dhahabu baada ya kuzuiliwa kwa takribani mwezi mmoja na Tume ya Madini TanzaniaTaarifa iliyotolewa na Acacia inaeleza sasa wataanza kusafirisha madini kutoka North Mara baada ya kutimiza masharti

Hata hivyo, Tume ya Madini imesema inaamini baadhi ya vipengele vya kanuni ya madini ya mwaka 2010 vilikiukwa na imewataka kuwasilisha mpango wa uchimbaji na ripoti ya upembuzi yakinifu ifikapo Ijumaa ya wiki hii

Acacia imekuwa kwenye mvutano wa muda mrefu na Serikali baada ya kuzuiwa kusafirisha Makinikia nje ya nchi kwa madai ya kutolipa mrabaha stahiki

Post a Comment

0 Comments