ACHANA NA PRESHA ALIYONAYO LAMPARD, CHELSEA WAMEUPIGA MPIRA JANA

Klabu ya Liverpool chini ya kocha mjerumani Jurgen Klopp usiku wa jana wameibuka kidedea katika fainali ya UEFA SUPER CUP iliyofanyika kule Uturuki dhidi ya Chelsea kutoka ligi kuu ya Uingereza pia.

Hii huwa ni fainali inayozikutanisha timu zilizoshinda UEFA Champions League na UEFA Europa League ambapo Liverpool (mabingwa wa Champions league msimu uliopita) wakakutana na Chelsea (mabingwa wa Europa League msimu uliopita).

Wengi tulitegemea kuona Chelsea ikifungwa magoli mengi sana hapo jana kutokana na kuwa na Pre-season Mbovu + matokeo mabaya ya mechi ya kwanza ya Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester United ambapo walichapwa 4-0.Lakini tulichokiona jana kilikuwa tofauti sana. Chelsea walionyesha kujiamini, ukomavu, uzoefu na kutaka kushinda pia. Hizi takwimu hazionyeshi wala kutuambia kama Chelsea ni dhaifu bali zinatuambia kuwa Chelsea wana uwezo wa kucheza hata na Manchester City na wakatoa DRAW au kushinda pia.

Jiulize tu tangu umeifahamu Liverpool ya KLOPP, ni timu gani ina uwezo wa kupiga pasi kwa kiwango kinachokaribiana nao? Vipi kuhusu idadi ya mashuti langoni? Vipi kuhusu kuichezea NUSU UWANJA Liverpool? Pass Accuracy je? Hayo yote jana yametokea na kutushangaza.

Ningeruhusiwa nichague mchezaji gani apewe ile tuzo ya mchezo wa jana kabla ya penati ningempa Ngolo KANTE. Jana Kante alikuwa katika ubora wake sana. ALIKUWA KILA MAHALI kama kawaida yake. Alikuwa akiendeleza harakati za kamati ya roho mbaya uwanjani akiKATA UMEME kila mahali. Acha kabisa aiseee

UEFA SUPER CUP
Mchezaji Ngolo Kante (blue) akiwatoka viungo na mabeki wa Liverpool hapo jana.

Kwa kumalizia niseme kwamba pamoja na kutokuwa washindi hapo jana, Chelsea wamedhihirisha ubora wao na waangaliwe kwa jicho la tatu. Wanaosema kuwa Kocha Lampard ataondoka kabla ya Christmas wanapaswa wafute kauli zao kwani watatushangaza wengi sana msimu huu. Ni hayo tu.

Post a Comment

0 Comments