ASAP ROCKY akutwa na hatia SWEDEN, atakiwa kulipa fidia hii...


Mahakama nchini Sweden imemkuta na hatia rapa Asap Rocky na wenzake wawili kwenye kesi ya kumpiga na kumjeruhi shabiki mmoja nchini humo mwezi June mwaka huu. Mahakama imeamua kutompa kifungo cha Jela (No Jail Time) lakini atamlipa baadhi ya fidia kijana huyo.

Mahakama imefikia hatua ya kutompa Rocky kifungo cha Jela licha ya kumkuta na hatia, ni kwa sababu walizozitoa kwamba shambulio lile halikuwa 'Serious' kiasi cha kuwashawishi kumfunga jela. 

Pia kutokana na muda aliotumia rumande kipindi chote akiwa Sweden mahakama imeamua kutomtoza faini bali kulipa fidia ya ($1300) sawa na Tsh. 3M kwa mlalamikaji. 

Post a Comment

0 Comments