BARIADI, SIMIYU: KATIBU TAWALA AKATAA WATUMISHI WA HOSPITALI KUNUNUA 'ULTRA SOUND' ILIYOIBIWA

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu (RAS), Jumanne Sagin ametengua uamuzi uliotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi (DC) wa kuwataka Watumishi wa Hospital ya Mji wa Bariadi kuchanga fedha ili kulipa kifaa hicho

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagin
Amesema "Tunarekebisha baadhi ya hatua zilizo tangazwa na DC jana. Jambo hili haliwezi likawa la kila mtu lazima tumtafute muhusika apatikane ili airejeshe au ashtakiwe."

Ameongeza "Haiwezekani watu 137 wote kwa pamoja wakaiba kifaa cha Ultra sound, wengine wapo katika sherehe za nanenane na wengine wapo likizo nyumbani."

Ameeleza kuwa "Kamanda afanye kazi yake na hatumfundishi. Serikali ina vyombo vya dola ambapo kuna watu wanalipwa kwa kazi ya uchunguzi."

Aidha, mmoja wa Wauguzi katika hospitali hiyo amesema "Tumeshukuru kwa msamaha uliotolewa kwa sababu tangu jana tumelala tuna presha. Mimi uwezo wangu ni mdogo, mshahara wangu ni mdogo."

Post a Comment

0 Comments