DRAKE AZIDI KUWEKA REKODI KWENYE CHATI ZA BILLBOARD, HII HAPA REKODI YAKE MPYA


Drake ametuamsha leo na taarifa hii mpya, album yake (Care Package) ambayo aliitoa kama zawadi kwetu mwezi uliopita imefanikiwa kukamata namba 1 kwenye chart za Billboard 200.Hii inakuwa album ya 9 kwake kushika nafasi hiyo ya kileleni. 

Kwa mujibu wa Billboard, Care Package yenye mikwaju 17 ambayo haikupata nafasi ya kutoka na kusikilizwa imeuza nakala 109,000 mpaka sasa. Pia hii ni album yake ya kwanza kushika namba 1 akiwa kwenye Label yake mpya OVO Sound. Zilizopita zote zilikuwa chini ya Young Money/ Cash Money/Republic.

Kingine kikubwa kwa Drake ni tattoo yake mpya mkononi. Drizzy ameichora picha maarufu ya kundi la The Beatles ambayo ilitumika kama Cover ya album yao (Abbey Road) ya mwaka 1969.

Sasa katika tattoo hiyo ya wanaume Wanne, Drake amejiweka mbele yao kuashiria kuwapita kwenye baadhi ya rekodi za Chart za Billboard ikiwemo ya Top 10 nyingi zaidi kwa mwaka, maingizo mengi zaidi kwa chart ya wiki na nyingine kibao. 

Post a Comment

0 Comments