KARDINALI PENGO ANG'ATUKA, ASKOFU MKUU RUWA'ICHI ASHIKA USUKANI KULIONGOZA JIMBO KUU DAR

Papa Francis ameridhia ombi la Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Tanzania, la kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Papa Francis amemteua Askofu mkuu mwandamizi Yuda Thaddeus Ruwa’ichiwa Jimbo kuu la Dar es Salaam, kuanzia sasa kuwa ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Hivi karibuni, Kardinali Polycarp Pengo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Miaka 75 tangu kuzaliwa kwake, aliwaambia watu washarika wa Jimbo kuu la Dar es Salaam kwamba, anasubiria wakati wowote kumtii Papa Francis atakapomwambia kupumzika katika utume wa Kiaskofu.

Post a Comment

0 Comments