MAREKANI YAIHIMIZA UINGEREZA IJITOE UMOJA WA ULAYA BILA YA MAKUBALIANO

Serikali ya Marekani inaunga mkono fikra ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano. Mshauri wa masuala ya usalama wa rais Donald Trump wa Marekani amesema alipokuwa ziarani mjini London wataunga mkono "kwa shauku", Uingereza ikijitoa katika Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano. 

Akizungumza na waandishi habari John Bolton amesema rais Donald Trump anategemea kuiona Uingereza ikijitenga na Umoja wa ulaya kwa ufanisi ifikapo Oktoba 31. 

Mshauri huyo wa rais anayeshughulikia masuala ya usalama ameongeza kusema rais Trump anatarajia kufikiwa makubaliano ya biashara kati ya Marekani na Uingereza. 

Kabla ya hapo John Bolton alikutana kwa mazungumzo pamoja na waziri mkuu Boris Johnson na viongozi wengine wa serikali ya Uingereza. 

Post a Comment

0 Comments