MWAKILISHI WA UPINZANI RWANDA ATOWEKA TANGU JULAI 15

Mwakilishi wa chama cha upinzani mashariki mwa Rwanda, Bw Eugène Ndereyimana hajulikani alipo kwa siku 30 sasa, tangu alipotoweka Julai 15 wakati akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano.Mke wake, Joselyne Mwiseneza amesema hajui kama mumewe yu hai au amefariki, na kwamba watoto wamebaki na huzuni kila siku wakiuliza wapi baba yao alipo.

Katika hali ya kushtua, kiongozi mwingine aliyekuwa akishika nafasi hiyo hiyo alitoweka mwaka 2016, na baadae mwili wake ulipatikana.

Katika habari nyingine, mwandishi wa habari wa TV1 Rwanda, Constantin Tuyishimire hajulikani alipo kwa siku 29 sasa, tangu alipotoweka Julai 16.

Idara ya Uchunguzi Rwanda (RIB) imedai mwandishi huyo huenda amekimbilia Uganda kutokana na kuwa na madeni mengi.

Awali mwandishi mwingine aliyetoweka 2016 na kurejea 2017 alisema alikuwa nje ya nchi.

Post a Comment

0 Comments